UJUMBE WA MENEJA MKUU 

UJUMBE WA MENEJA MKUU 

Mpango mkakati huu umeainisha malengo matano (5) ya kimkakati ya CEAMCU Ltd kwa miaka mitano ijayo (2026/27 – 2030/31) kama ifuatavyo:

  1. Utoaji wa Huduma kwa AMCOS Wanachama;
  2. Usimamizi wa Mali, Uwekezaji na kuongeza Uwezo wa Kifedha;
  3. Utendaji na usimamizi wa shughuli za chama;
  4. Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA);
  5. Ushirikiano wa Kimkakati

Lengo ni kuimarisha uendeshaji wa shughuli za Chama kwa maslahi ya AMCOS wanachama kwa kuzingatia misingi ya Uadilifu, Uwazi na Uwajibikaji, Ubunifu na Utaalam. Ni matumaini yangu kuwa mpango mkakati huu utakuwa chachu ya maendeleo ya CEAMCU Ltd kwa kuleta maendeleo yake na kwa AMCOS wanachama na kuongeza mapato yake kwa miaka mitano ijayo.

ANASIA CHARLES KIMAMBO

KAIMU MENEJA MKUU