Kuhusu sisi

Utangulizi

Central Zone Agricultural Cooperative Union (CEAMCU) Ltd ni Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida. CEAMCU Ltd kilichoanzishwa kwa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya Mwaka 2003 na kusajiliwa tarehe 05 Mei 2006 kwa usajili Na. 5567.

Kutokana na mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Ushirika nchini Tanzania, CEAMCU Ltd ilisajiliwa tena chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni zake za Mwaka 2015, kwa usajili Na. AFF-SGD-MAN-DC-2022-16 tarehe 15 Disemba, 2022.

Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa CEAMCU Ltd ni kuhudumia vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) vinavyojihusisha na shughuli za kilimo cha mazao ya aina mbalimbali hasa Tumbaku, Pamba, Korosho na mazao ya mikunde.

Historia na Maendeleo ya CEAMCU Ltd

Central Zone Agricultural Cooperative Union (CEAMCU) Ltd ni Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida kilichoanzishwa kwa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya Mwaka 2003 na kusajiliwa tarehe 05 Mei 2006 kwa usajili Na. 5567. Kutokana na mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Ushirika nchini Tanzania, CEAMCU Ltd ilisajiliwa tena chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni zake za Mwaka 2015, kwa usajili Na. AFF-SGD-MAN-DC-2022-16 tarehe 15 Disemba, 2022.

Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa CEAMCU Ltd lilikuwa ni kuhudumia vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) vinavyojihusisha na shughuli za kilimo cha mazao ya aina mbalimbali hasa Tumbaku, Pamba, Korosho na mazao ya mikunde. Malengo mahsusi ya kuanzishwa kwa CEAMCU Ltd ni kama ifuatavyo: –

  1. Kutafuta na kusambaza taarifa ya masoko ya tumbaku na mazao mengine kwa lengo la kuwezesha mazao hayo kuuzwa kwa bei nzuri kwa faida ya wanachama wake;
  2. Kuagiza na kusambaza pembejeo za kilimo kwa wanachama wake kwa bei nafuu ili kuboresha mazao ya tumbaku, pamba, korosho na mazao ya mikunde;
  3. Kuanzisha na kuendeleza mitandao imara ya kilimo bora cha tumbaku, korosho, pamba na mazao ya mikunde;
  4. Kushauri na kutoa elimu ya Ushirika kwa wanachama wake ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa vyama wanachama na kuwaendeleza watendaji wake kuhusu shughuli zake ili kuimarisha uchumi wake;
  5. Kumiliki, kukodi na kustawisha ardhi, majengo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi yake na wanachama wake;
  6. Kuwezesha uendeshaji wa vyama vya msingi wanachama kwa kutoa ushauri na huduma mbalimbali za kiushirika kama ilivyoainishwa kwenye masharti yake;
  7. Kuwakilisha wanachama katika mikutano ya chama kilele, Bodi/taasisi na mabaraza ya mazao.
  8. Kuhamasisha na kujenga ufahamu wa wanachama kwa kuwawekea misingi na miongozo itakayohakikisha ubora wa tumbaku, pamba, korosho na mazao ya mikunde;
  9. Kuwezesha shughuli za utafiti wa mazao ya tumbaku, pamba, korosho na mazao ya mikunde;

Hadi kufikia tarehe 31 Machi 2025, CEAMCU Ltd ilikuwa inahudumia vyama vya msingi (AMCOS) wanachama 46 (30 vyama wanachama na 16 visivyo vyama wanachama) kutoka Wilaya za Manyoni na Itigi vyenye zaidi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha tumbaku, pamba, korosho na mazao ya mikunde. Bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na CEAMCU Ltd zimekuwa zikichochea maendeleo binafsi ya wanachama wa vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) na kuboresha ustawi wa kiuchumi na kijamii.

TOP